Lyrics

Umoja ni fahari yetu Undugu ndio nguvu Chuki na ukabila Hatutaki hata kamwe Lazima tuungane, tuijenge nchi yetu Pasiwe hata mmoja Anaetenganisha Naishi, Natumaini, Najitolea daima Kenya, Hakika ya bendera Ni uthabiti wangu Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani Daima mimi mkenya Mwananchi mzalendo Kwa uchungu na mateso Kwa vilio na uzuni Tulinyakuliwa Uhuru na mashujaa wa zamani Hawakushtushwa na risasi au kufungwa gerezani Nia yao ukombizi kuvunja pingu za ukoloni Naishi, Natumaini, Najitolea daima Kenya, Hakika ya bendera Ni uthabiti wangu Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani Daima mimi mkenya Mwananchi mzalendo Wajibu wetu Ni Kuishi kwa upendo Kutoka ziwa Mpaka pwani Kaskazini na kusini Naishi, Natumaini, Najitolea daima Kenya, Hakika ya bendera Ni uthabiti wangu Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani Daima mimi mkenya Mwananchi mzalendo
Writer(s): Eric Wainaina Lyrics powered by www.musixmatch.com
Get up to 2 months free of Apple Music
instagramSharePathic_arrow_out