Lyrics

(Wewe) mh (wewe) Mmh (wewe, mh-ah, wewe) Spana, ah-mh Shy town boy (mh) Niko na Drama boy (mh) (Jey Drama on the beat) Ah, hi, hi, hi, Huddah Uhali gani we msaliti haufai Yuda, nimeona leo nikusabahi nainai Nilikuhongaga mpaka saa, na bado ukanipotezea muda Ah, penzi lako kama lift ukanishushua njiani Hukuamini kuna siku mziki utanipa ramani Ukapata mchizi asiye na dhiki na akakuweka ndani Hivi hukujua nyumba ya ridhiki mpangaji Ilinitouch sana iliniumiza sana, ilinifanya nikakesha usiku na mchana Haukuwa fungu langu kwahiyo sikuweza kung'ang'ana Kisicho ridhiki hakiliki hata kikiungwa na nyanya Vipi, mchizi yupo? Mbona siku hizi hampostiani tena Makopa kopa lnstagram hamkomentiani tena Mtaani hatuwaoni mkiongozana tena Sitaki amini ka' na yeye tayari mmeshaachana tena Nisingekuwa mstaamilivu Huwenda duniani leo nisingekuwepo Ulinipa maumivu, niliamini siwezi kupona leo wala kesho Namshukuru Mungu, kwa kunifutia kumbukumbu zako Maana niliishi na maumivu Mwili ukawa kijivu, nikawa ni kichekesho Sikulaumu wewe (wewe), sikuombei magumu wewe (wewe) Mungu akurehemu wewe (wewe) Unayoyafanya kwangu yasijirudie kwako, oh Ooh, mh Ah, usidhani nakuchukia, mi' sikuchukii (mi sikuchukii) Hizi salamu tu nakutumia Hata mapenzi yako mi' sikumbukii (hata mapenzi yako mi' sikumbukii) Uliacha mbachao kwa msala upitao, kunikalia vikao haisaidii Naskia ukinionaga kwa TV, unatamani urudi ila mimi ndo sifikirii Ah, mshedede siku hizi na vichenchede Mambo yako yedede, bata kila deide Mafekeche debe daily tukiplay dede Si ulisema sina future maisha nimeyamedede Ah, najiona mbali, siku mziki umeshaanza kunilipa Nashukuru Mungu bwana, kila kona nasikika Kila dakika kote nafika Na kwenye show siendi na dyaba, nakuwaga mapipa Jangwani uliniacha mpenzi Ukaenda mbali nami, ukafuata wenye maji mengi Angani kuna nini mpenzi Ulichagua maisha ya ndege kuruka kuspend Utu, utu wangu niliwekeza kwako utu Utu, utupu wako ulimuonyesha mwenye pesa Akaenda na we, eh, we Nisingekuwa mstaamilivu Huwenda duniani leo nisingekuwepo Ulinipa maumivu, niliamini siwezi kupona leo wala kesho Namshukuru Mungu, kwa kunifutia kumbukumbu zako Maana niliishi na maumivu Mwili ukawa kijivu, nikawa ni kichekesho Sikulaumu wewe (wewe), sikuombei magumu wewe (wewe) Mungu akurehemu wewe (wewe) Unayoyafanya kwangu yasijirudie kwako, oh Take five now (take five now)
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out