Lyrics

Baba kaja na swali mama kanipa jibu ili niulizwe swali, eeh! swali x2 Asanteni kwa kuja ndugu zangu, marafiki zangu asanteni kwa kuja majirani zangu asanteni kwa kujax2 oyo oyoo ndugu zangu, jamaa na marafiki zangu, waneni husema, usimuhadithie mtu ndoto yako ya jana usiku, lakini hapa ni kinyume siri tunasema bayana tunaficha poleni sana kwa kuja, najua... wakati ni mali, wakati ni ukuta kama neno litokalo mdomoni kama sauti na pengine ni kama moshi ukitoka haurudi lakini kwanini dobi kutakasa kaniki ali tunajua rangi ya nguo ndugu zangu ukiona paka kakubali kulala chari anza kuomba ruhusa kazini najua, mila na desturi za kwetu huruhusiwi kusema, utaambiwa una gubu una hila uchuro, huna malezi ya pande mbili na kama watakuwa wamechukia sana watasema uliaza kutoka miguu badala ya kichwa yaani huna adabu asanteni sana kwa kuja, mimi sikuwa naijuwa safari hii kabla japo niliitegemea sana wazazi wangu waliwahi kuniambia kuwa ipo siku nitasafiri, nilicheka sana lakini wao walicheka mara mbili, walinitazama kisha wakacheka tena mara ya tatu, tena kwa nguvu, basi kama tofauti ya vicheko vyao nilingelijua usiku wa jana kabla ya leo nadhani ningeudhihirishia uma ule usemi wa kuwa, riziki ni kama ajali, hauitambui siku ya kuja, cha kushangaza baba alishika swali, mama akanipa jibu niulizwe swali Je ungependa kuona nini unapokuwa safarini mwanetu kipezi? mama akasema mwambie ungependa kuona miti inavyorudi nyuma wakati wa safari ningependa kuona miti inavyorudi nyuma wakati wa safari gudi gudi gudi sana kiziwanda wetu nini tena kiziwanda wetu? mwambie, ungependa ule wakati wa uchimbaji dawa kati kati ya safari ningependa ule uchimbaji dawa kati kati ya safari, ha ha ha ha! wao umekuwa kiziwanda wetu oy oyoo asanteni kwa kuja x4 haa; ndugu zangu kwa sasa sicheki nakumbuka majibu yangu ya kupewa, poleni sana kwa kuja nawapa pole wote kwa kufunga maduka yenu kuahirisha shughuli zenu za lazima, kuwadanganya waajiri wenu ili tu mnisindikize ndugu yetu, aidha kuogopa lawama mtaani pia labda kujua safari huwa inaazaje, yote ya yote nasema asanteni japo neno hili halina maana tena siku hizi nafurahi James kukuona tena huku mbele kama sijakosea kuhesabu umebeba mara sita umempita hata kasim pale nyuma, yeye amebeba mara tano, muda mwingi alikuwa abapiga zogo na kuuliza, tatizo lilikuwa nini mpaka naenda? Sadiki sikumuona kubeba ila namuona kama hana raha tena mwenye haraka wakati naandaliwa aliniuliza peter na Juma huwa inachukua muda gani mpaka safari kumalizika eh! eh! oyo oyoo, ndungu zangu atupaye tupe humrudia mwenyewe, naomba mpunguze mwendo mzee mpiri siwezi kumlaum maana umri umepita sasa oyo oyoo naomba msiende mbio, mtamuacha wakati na yeye ana nia ya dhati, kushuhudia safari ya pili, mh; mh! nilikipenda sana kile kikao cha jana cha kuamua leo ndio niende kula kunywa, gharama kwangu gharama kwangu nitatoa mimi maana nina uchungu kweli! kweli ndio fimbo ya kumkamatia muovu. Baba kaja na swali mama kanipa jibu ili niulizwe swali, eeh! swali x2 asanteni, ndugu zangu kwa kuja marafiki zangu asanteni kwa kuja majirani zangu, asanteni kwa kuja oyo oyoo, asante kwa kuja x2 oyo oyoo oyoo oyoo oyo oyoo End#########
Lyrics powered by www.musixmatch.com
Get up to 2 months free of Apple Music
instagramSharePathic_arrow_out