Lyrics

Intro – Yeah Hii ni habari njema Hii ni moja ya ngoma inayowakilisha vyema Hisia za mtu aliyetemwa Naheshimu tabia nyingi za vijana Ila sio za kuziendekeza sana Kama kupenda ni mtihani wa kila kijana Kaza! [Verse 1 – Na mawazo kichwani, uko wapi hivi kwani? Navyoku-miss hadi nalia, naishia kukuona pichani Uzuri wako umeni-cost, mi dai sio ka dukani Ukiniona nime-lost, nishakosa ramani Napenda kujizuia nisiwe hata nakuwaza Niliyempenda amekimbia, sijui nlishindwa kumkataza Nimebaki naugulia, sina hata wa kuniliwaza Ka sipo ndani ya dunia, kote kumenyamaza Sa nimepata mwenye figure, ila huyu anaringa Anaringa on every finger Walompa washaanza kuniwinda Dah, ulikuwa ukitabasamu, sio tu kwenye good times Umeniacha nina hamu baada ya kunionjesha utamu Na nahisi hiyo figure ulionekana hata umekaa Ba-basi nilifika ila nikakosa pakukaa Roho inahuzunika na furaha imekwisha [Hook – Nikisema niko busy, hujali Nsipopiga simu usiku, hujali Nkikwambia sina kitu, unasema nsijali Nkafurahi kila siku nlihisi nimepata zali Nikisema niko busy, hujali Nsipopiga simu usiku, hujali Nkikwambia sina kitu, unasema nsijali Ila hatari mwisho wa siku umekwenda mbali [Verse 2 – Maji ya moto kwa baridi ina maana hamna joto Hata mtoto kwa mkaidi si kwamba hamna mboko Kukupenda nilijitahidi ila umeniacha kwenye chocho Sijui akili ulinizidi au ndo hivyo niko soso Si wakati tunapendana, haya tulishayaongea Ikawa tuombe kwa Maulana tu yasije kutokea Leo wapi ulipoelekea, hadi usahau ulipotokea? Nakupenda honey, nateswa na haya mazoea Mapenzi mnapopendana, ushenzi mnapotengana Kuwa crazy inawezekana, kwa wezi walivyojazana Umeniacha sina amani wala raha, niko ndani Niende studio, nampigia Mbezi, wapi hapatikani! Huenda mi nilikupenda, ila we ulinitamani Kweli umenipenda ila unapoenda ni gizani Unafeli (mama!) au umepandwa na shetani? Kweli siko sawa? Nambie nakosa gani [Hook – Nikisema niko busy, hujali Nsipopiga simu usiku, hujali Nkikwambia sina kitu, unasema nsijali Nkafurahi kila siku nlihisi nimepata zali Nikisema niko busy, hujali Nsipopiga simu usiku, hujali Nkikwambia sina kitu, unasema nsijali Ila hatari mwisho wa siku umekwenda mbali [Verse 3 – Mapenzi yangu gado Kuchoshwa na mpenzi wangu bado Ah, ila mwenzangu hufagilii Navuta waya, natupa text hufatilii Ah, basi mi yangu macho Na nitafutwa na ndugu zangu jasho Ah, napigwa jiwe na Young Dee Kwa sababu ya mapenzi, crazy, baby! [Hook – Nikisema niko busy, hujali Nsipopiga simu usiku, hujali Nkikwambia sina kitu, unasema nsijali Nkafurahi kila siku nlihisi nimepata zali Nikisema niko busy, hujali Nsipopiga simu usiku, hujali Nkikwambia sina kitu, unasema nsijali Ila hatari mwisho wa siku umekwenda mbali [Outro – Nimenasa mpenzi, umenikimbia Umeniacha kipenzi, wapi ntakimbilia? Nimedata kishenzi, ah ka umeshtukia Maana sitaki kufikiri ulikuwa ukiniibia Nimenasa mpenzi, umenikimbia Umeniacha kipenzi, wapi ntakimbilia? Nimedata kishenzi, ah ka umeshtukia Maana sitaki kufikiri ulikuwa ukiniibia
Lyrics powered by www.musixmatch.com
Get up to 2 months free of Apple Music
instagramSharePathic_arrow_out